Wapiganaji wa al-Shabaab nchini Somalia 
Wanachama wa kundi la al-Shabaab nchini Somalia wanasema kuwa mji wao kusini mwa Somalia umeshambuliwa na wanajeshi wa mataifa ya Magharibi.

Wapiganaji hao wanasema wanajeshi wazungu waliuvamia mji wa Barawe usiku wa manane.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema mpiganaji mmoja aliuwawa na risasi nyingi zilifyatuliwa.
 
Baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa helikopta ilitumiwa kwenye shambulio hilo.
Wengine wanaeleza kuwa wanajeshi waliingia usiku wakitokea pwani.

Kundi la al Shabaab limesema kuwa lilifanya shambulio la mwezi uliopita mjini Nairobi dhidi ya jumba la maduka ambalo kwa sehemu linamilikiwa na Muisraili.

Miaka mine iliyopita jeshi la wanamaji wa Marekani liliuvamia mji wa Barawe kumuuwa mtu aliyeshukiwa kuwa mfuasi wa Al-Qaeda.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top