Kikao cha AU 
Viongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, wamekubaliana kuwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya asihudhurie kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, ila ikiwa itaahirishwa.

Katika azimio lao viongozi wa Afrika walisema kuwa kiongozi yeyote wa taifa asishitakiwe kuhudhuria mahakama yoyote ya kimataifa wakati yuko madarakani.

Kesi ya Rais Kenyatta ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu inatarajiwa kuanza mwezi ujao mjini Hague, ingawa ameomba mara kadha kwamba iahirishwe.

Bwana Kenyatta siku zote amekuwa akisema kwamba atashirikiana kikamilifu na ICC.

AU inaishutumu ICC kuwa na kigeugeu - kwamba inawashtaki Waafrika na siyo watu wa mataifa ya magharibi.

Hapo awali Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn, alisema kesi za ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na Omar al-Bashir wa Sudan zinaweza kuzuwia juhudi za kuleta amani na mapatano katika nchi zao.
Mkutano huo umemalizika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

1 comments:

Anonymous said... October 13, 2013 at 8:16 AM

hiki ni chombo cha ovyo tu hapa duniani kupoteza hela za wapiga kura kujadili ujinga...Unajitoa kwenye mikono ya sheria halafu..utawala wa sheria na democrasia utauenezaje nchini mwako...do they think dunia itawaachia waue watu kwa uroho wa madaraka na mali walio nao...hawa wanachemka ICC will be thr forever na itawafikia tu..hata wapitishe maresolutions ya namna gani.

 
Top