Wafuasi wa serikali ya Bashar Al Assad
Rais wa Marekani Barack Obama, amesema kuwa atafanya
juhudi zaidi za kidiplomasia kuangamiza zana za kemikali za Syria ingawa pia ameliambia jeshi lake kuwa tayari kuchukua hatua ikiwa juhudi
zake zitafeli.
Kwenye hotuba yake, Obama alisema kuwa
amelitaka baraza la Congress kuakhirisha kura yake kuhusu kutumia nguvu
za kijeshi dhidi ya Syria.
Marekani imetishia kufanya
mashambulizi ya angani baada ya shambulizi la kemikali kuwaua mamia ya
watu mjini Damascus mwezi jana.
Urusi imependekeza kuwa silaha hizi ziwekwe chini ya udhibiti wa jamii ya kimataifa.
Ingawa maafisa wa Syria wamekubali kutii agizo
la Marekani, nchi hiyo pamoja na washirika wake wana wasiwasi ikiwa
Syria itafanya kama inavyosema.
Mpango wa Urusi ulisababisha siku moja ya mashauriano mazito ya kidiplomasia katika Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.
Akiongea katika Ikulu ya White House, Obama
alisema kuwa serikali yake, ilikataa wito wa kuchukua hatua za kijeshi
dhidi ya Syria kwa sababu haamini ikiwa kutumia nguvu itasuluhisha
mgogoro huo.
Lakini alisema kuwa alibadili msimamo wake baada
ya zana za kemikali kutumiwa kwenye mashambulizi katika viunga vya mji
wa Damascus tarehe 21 mwezi Agosti.
"usiku huo, dunia nzima iliona kwa kina athari
mbaya za zana za kemikali na kwa nini watu wengi duniani wanahisi kuwa
zana hizo hazipaswi kabisa kutumiwa, ni uhalifu dhidi ya binadamu na
ukiukwaji wa sheria za vita,'' alisema Obama.
Serikali ya Syria imekanusha kuwa ilitumia
silaha za kemikali kushambulia watu na badala yake imelaumu waasi
ikisema walizitumia katika juhudi zao za kutaka kumng'oa mamlakani Rais
Bashar al-Assad
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment