HATUA ya Rais Jakaya Kikwete kuamua kutafuta suluhu na Rais wa Rwanda,
Paul Kagame, kupitia kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC), Rais Yoweri Museveni wa Uganda, imeacha wingu la mashaka kama
kiongozi huyo ataweza kuleta muafaka katika mgogoro uliojitokeza baina
ya wakuu hao wawili.
Mapema wiki iliyopita, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
alisema, Rais Kikwete amemuomba Mwenyekiti wa EAC, Rais Museveni
kusuluhisha mgogoro uliojitokeza kati yake na Kagame, baada ya kumpa
ushauri wa kukaa meza moja ya mazungumzo na waasi wa FDRL.
Hata hivyo, wadadisi na wafuatiliaji wa mambo waliozungumza na MTANZANIA Jumatano kwa nyakati tofauti, wameeleza sababu kadhaa ambazo zinamuondolea sifa Rais Museveni kusuluhisha mgogoro huo.
Sababu zote zinazotajwa zinajengwa na msingi wa uhusiano wa kihistoria pamoja na matakwa yanayofanana kati ya Rais Kagame na Museveni.
Ingawa Tanzania nayo inatajwa kuwa nyuma ya urafiki na Museveni, ikiwa ni pamoja na kufanikisha jambo zito la urais wake, lakini si kwa kiwango kama kile kinachotajwa kwa Kagame.
Kwamba ni Kagame ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, amekulia Uganda baada ya familia yake kukimbilia huko kutokana na mapinduzi yaliyosababisha kukomeshwa kwa utawala wa Kitutsi.
Ni katika hali hiyo, inaelezwa kuwa miaka ya 1980, Kagame alipigana ndani ya Jeshi la waasi la Yoweri Museveni, na baadaye kuwa ofisa wa Jeshi la Uganda, baada ya ushindi wa kijeshi uliompatia urais, Museveni.
Misingi hiyo ndiyo ambayo inawafanya wachambuzi wamuone Kagame kuwa ni mtoto wa nyumbani zaidi nchini Uganda tofauti na Tanzania.
Jambo lingine ambalo linadhihirisha kuwapo kwa ushahidi huo wa uswahiba, ni urais wa Kagame nchini Rwanda, kuanzia kuingia hadi kuitawala kwa ushindi wa kijeshi akitokea Uganda, baada tu ya kujiunga na kundi la Rwandan Patriotic Front (RPF), ambalo lilivamia nchini humo mwaka 1990.
Wadadisi na wafuatiliaji wa mambo ambao wanautizama kwa sura tofauti msimamo wa Rais Kikwete kutaka Museveni awe msuluhishi kwenye mgogoro wake na Rais Kagame, pia wanaitaja sababu nyingine ambayo inaweza kuwa kikwazo cha kutofikia muafaka, kwamba inachagizwa na ushirika wa majeshi ya Rwanda na Uganda yaliyojipenyeza ndani ya makundi ya waasi wanaopigana na Serikali ya Kongo, huku yakiwa na matamanio yanayofanana ya kuchuma utajiri mkubwa wa madini katika eneo la Mashariki ya nchi hiyo pamoja na kutekeleza vitendo vya kinyama dhidi ya binadamu.
Kwa nyakati tofauti, Uganda na Rwanda, ziliwahi kushutumiwa kuwa nyuma ya vikundi hivyo vya waasi vilivyoko mashariki mwa Kongo.
Wanaozungumzia hilo wanasema kwamba, kitendo cha Rais Kikwete ambaye ameamua kutoa jeshi lake kupambana Kongo dhidi ya vikundi vya waasi hao, kinapingana na maslahi yanayofanana ya Museveni na Kagame.
Kutokana na hilo, wengi wanaona kwamba, Museveni si mtu sahihi wa kutatua mgogoro uliojitokeza baina ya Rais Kikwete na Kagame.
Wanaosema hivyo wanajenga hoja kwamba, ni rahisi Museveni kumtosa Kikwete ukilinganisha na Kagame.
Kwamba ushahidi wa hilo, unathibitishwa pia jinsi ambavyo Uganda ilivyohangaika kuipigia chapuo Rwanda, kutaka iingizwe kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakati wa mchakato wa kuiunda mwaka 1999, baada ya kuvunjika ile ya mwaka 1977, ambayo kuvunjika kwake kulitokana na sababu za migogoro kama hii inayojitokeza sasa ya kisiasa na kiuchumi.
Ni Uganda ambayo iliibua hoja ya kutaka Rwanda iingizwe ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika kikao kilichoketi Januari mwaka 1999.
Licha ya hoja hiyo kuibua moto mkali, lakini Tanzania ilikataa ikieleza kwamba, ilikuwa haiwezekani kuwaingiza wanachama wapya katika hatua changa iliyokuwa nayo EAC.
Hata hivyo hoja hiyo ya Uganda ilishindwa baada ya Tanzania na Kenya kupiga kura ya kupinga, ingawa baadaye hoja ya Uganda ikashinda na Julai 6, 2009, Burundi na Rwanda zikajiunga EAC.
Pamoja na hayo, kuwepo kwa taarifa za sasa za kusainiwa kwa mkataba wa kiusalama wa kusaidiana kijeshi kati ya nchi tano, ambazo ni Ethiopia, Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini, endapo mmoja wao watavamiwa, nazo zimeacha wingu la mashaka kama kiongozi yeyote toka katika nchi hizo anaweza kuwa mtu sahihi wa kusuluhisha mgogoro kati ya Kikwete na Kagame, wakati ambapo Tanzania majeshi yake yanapambana na waasi walioko Kongo.
Katika tathimini kuhusu uzito wa ushirika huo wa Museveni na Kagame, zipo taarifa zinazodai kuwa tayari Serikali ya Tanzania imeanza kufikiri kubadili uamuzi wake wa kutaka Museveni awe msuluhishi wa mgogoro huo.
Gazeti hili limedokezwa kuwa tayari Serikali inataka kuupeleka mgogoro huo kwa Rais mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano au Umoja wa Afrika (AU).
Rais Kikwete alijikuta katika vita ya maneno na Rais Kagame, kwa sababu tu ya ushauri aliompa mwezi, Mei mwaka huu, wakati wakiwa kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) wa kumtaka akae meza moja ya mazungumzo na waasi wa kundi la FDRL, wanaoaminika kufanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Tangu hapo ni upande wa Rwanda, ambao umekuwa ukitoa maneno ya vitisho na kashfa dhidi ya Rais Jakaya Kikwete pamoja na familia yake.
Hali hiyo kwa kiwango kikubwa, imechochea kukua kwa uhasama baina ya mataifa haya mawili.
Uhasama ambao umeshuhudia vita ya kiuchumi na kimakundi ndani ya Jumuiya ya EAC na hivyo kutishia mustakabali wake.
Tayari Uganda, Rwanda na Kenya zinaonekana kujitenga na Tanzania na kuanzisha kile kinachoonekana kuwa ni umoja wao, kwa kupanga mipango ya pamoja ya kiuchumi, kama kuanzisha reli ambayo itatoka katika Bandari ya Mombasa kupita Uganda hadi Rwanda, ambayo itakamilika mwaka 2017.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment