Gehad al-Haddad ni mtoto wa mshauri wa zamani wa Mohammed Morsi kuhusu maswala ya kigeni
Msemaji rasmi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood amekamatwa nchini Misri.
Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ambapo inasemekana kuwa Gehad al-Haddad alikamatwa akiwa na mwanachama mwingine mmoja wa vuguvugu hilo katika nyumba moja mjini Cairo.
Bwana Haddad aliwahi kuhudumu kama
afisa wa ngazi ya juu wa naibu mkuu wa majeshi, Khairat al-Shater, wa
vuguvugu hilo na kawaida alizungumza na vyombo vya habari vya kigeni.
Serikali ya Misri imekuwa ikifanya msako dhidi
ya makundi ya kiisilamu tangu jeshi kumwondoa mamlakani aliyekuwa rais
Mohammed Morsi mwezi Julai.
Awali, mahakama ya uhalifu mjini Cairo, iliamua
kuwa mali zote za viongozi wa vuguguvu hilo pamoja na lile la Gamaa
Islamiya kupigwa tanji.
Viongozi wa mashtaka waliwaekea vikwazo maafisa
wa ngazi ya juu wa Brotherhood akiwemo, Mohammed Badie, Shater na
wengine wengi mnamo mwezi Julai ambapo wengi wao wamezuiliwa kuhusiana na madai ya kuchochea ghasia na mauaji.
Mamia ya watu wanataka Bwana Morsi kurejeshwa mamlakani , wengi wakiwa wanachama wa Brotherhood .
Aidha makabiliano yaliyotokea mwezi jana kati na
polisi na wafuasi wa Morsi yalisababisha vifo vya wanachama wengi pale
polisi walipovamia kambi zao mbili walipokuwa wanataka Morsi kurejehswa
mamlakani.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment