Polisi wa Uhispania wanasema kwamba wamelikamata genge linalosafirisha wahamiaji kimagendo ambapo watu 75 wametiwa mbaroni Uhispania na Ufaransa.
Msemaji alieleza kuwa genge hilo likiwasafirisha
raia wa Uchina na kuwaingiza kimagendo katika nchi za Ulaya na
Marekani, na kila mkimbizi akilipa kama Euro 50,000 kwa safari hiyo.
Polisi wanasema viongozi wa genge hilo Ulaya waliokuwa na makao yao mjini Barcelona, ni kati ya wale waliokamatwa.
Polisi pia wamekuta paspoti zaidi ya 80 za nchi kama Japan, Hong Kong na Singapore.
Chanzo: BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment