Dk Mushi
Kufuatia
sakata kuwa Serikali haina mitaala rasmi ya kufundishia shuleni,
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Dk Paul Mushi,
amejiuzulu wadhifa huo.
Nafasi yake imechukuliwa na Mkurugenzi wa Idara ya kubuni na kuendeleza Vifaa vya Elimu, Dk Leonard Akwilapo.
Akihojiwa na NIPASHE kwa njia ya simu jana jijini Dar es Salaam, Dk. Mushi alithibitisha kujiuzulu na kusema alichukua hatua hiyo kwa hiari yake bila kushinikizwa na mtu, “Hakuna aliyenishinikiza nimeamua mwenyewe kuandika barua ya kujiuzulu,” alisema Dk Mushi
Kaimu Mkurugenzi Dk Akwilapo alipohojiwa juu ya mtangulizi wake aliyeachia ngazi , Alhamisi wiki hii, alisema aliondoka kwa maamuzi yake mwenyewe bila shinikizo kama alivyoeleza, “Sio siri ni kweli amejiuzulu na aliniambia ni maamuzi yake aliyoyafanya ya kujivua madaraka ya Mkurugenzi Mkuu bila ya kugombana na mtu na juzi ndio alipewa barua yake na mimi kupatiwa barua ya kuwa kaimu,” alisema Dk Akwilapo
Katika mkutano wa Bunge la mwezi huu, Mbunge wa kuteuliwa na Rais James Mbatia (NCCR-Mageuzi), aliwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu hapa nchini.
Katika hoja hiyo, alilaumu kutokuwapo kwa mitaala inayoongoza ufundishaji wa masomo shuleni hali inayosababisha kudorora kwa elimu. Kadhalika aliibua tuhuma za uchapishwaji wa vitabu ambavyo maudhui yake hayana viwango pia waliopewa kazi ya kuchapisha ndiyo hao waliokuwa wahariri na waandishi. Pia alihoji sababu za uchapishaji wa vitabu hivyo kufanyika nje ya Tanzania hali ambayo inasababisha kuwapo kwa matumizi mabaya ya fedha.
Katika kujibu hoja hizo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alilithibitishia Bunge kuwa serikali ina mitaala na nakala zake ziliwasilishwa bungeni na hoja hiyo ikazimwa. Baada ya kuwasilishwa kwa mitaala hiyo, bunge iliunda kamati ya kujiridhisha kama ni kweli mitaala hiyo ni sahihi ambapo ilikuja na majibu ya kujiridhisha kuwa ni ya kweli.
Hata hivyo, kwa upande wa James Mbatia alisema bado kuna utata katika mitaala hiyo licha ya kamati hiyo kujiridhisha kuwa mitaala ipo sahihi.

0 comments:
Post a Comment