Shirika la Umoja wa mataifa linalokabiliana na dawa za kulevya na uhalifu UNODC limesema kuwa kumekuwa na upungufu mkubwa katika utengenezaji na uuzaji wa dawa za kulevya.

Shirika hilo limesema kuwa usambazaji wa dawa aina ya Cocaine duniani umepungua maradufu. Bethany Bell ametutumia taarifa hii kutoka Vienna.

Ripoti hiyo ua Umoja wa mtaifa inasema kuwa dawa zinazotengenezwa kutokana na zao la Opium kama vile heroin ndizo zinazosababisha maafa makubwa zaidi na maambukizi ya magonjwa mengi duniani.

Japo shirika hilo limesema kuwa kumekuwa na ongezeko la zao Opium nchini Afghanistan kwa mwaka wa tatu mtawalia inaonekana usambazaji na utumiaji wa Cocaine duniani umepungua.

Hata hivyo shirika hilo limeonya kuwa kuna ongezeko katika ain ampya ya dawa za kulevya na utumiaji mkubwa zaidi wa dawa hizo umeripotiwa katika mataifa ya Amerika ya kaskazini.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top