Rais wa Kenya uhuru Kenyatta ndiye Rais anayejishughulisha zaidi kwenye mtandao wa Twitter barani Afrika.
Kenyatta amempiku Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Kenyatta ambaye amekuwa mamlakani tu
kwa mwaka mmoja, amejipatia wafuasi 456,209, yuko mbele ya mwenzake wa
Rwanda Paul Kagame mwenye wafuasi 408,353 ambaye amekuwa mamlakani tangu
mwaka 2000, miaka sita kabla hata ya Twitter kuanzishwa.
Rais wa Afrika Kusini anayesifika kwa kashfa mbali mbali, Jacob Zuma ana wafuasi 325,896 akishikilia nafasi ya tatu.
Hata hivyo swali ni je maerais hawa hutumia vipi Twitter? Je wao huwa na mazungumzo ya moja kwa moja na wafuasi wao?
Waziri mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi
'@AmamaMbabazi,' ndiye kiongozi mwenye kuwasiliana zaidi na wafuasi wake
duniani kwenye Twitter huku akiwajibu maswali yao kwake.
Asilimia tisini na tano ya mawasiliano yake
kwenye Twitter ni '@replies,' ishara ya kuwajibu wafuasi wake. Utafiti
huu ni kwa mujibu wa utafiti wa kimataifa kuhusu viongozi
wanavyojishughulisha na Twitter, wenye mada, Twiplomacy.
Waziri mkuu mpya wa India, Narendra Modi ana
wafuasi milioni 4,967,847 , na anaelekea kushinda Ikulu ya white House
ambayo ina wafuasi milioni 4,976,734 katika nafasi ya tano.
Zaidi ya asilimia 83 ya mataifa yote duniani
yana uwakilishi katika Twitter, na asilimia 68 ya viongozi wana akaunti
za twitter kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Burson-Marsteller, nchini
Marekani.
Viongozi wanaofuatwa sana kwenye Tiwtter ni
pamoja na Barack Obama (@BarackObama) akiwa na wafuasi milioni 43, Papa
Francis (@Pontifex) ana wafuasi milioni 14 akifuatiwa na Rais wa
Indonesia Susilo Bambang Yudhoyono (@SBYudhoyono) akiwa na wafuasi
milioni tano.
Rais Barack Obama alikuwa kiongozi wa kwanza kuanzisha akaunti ya Twitter mwaka 2007.
Kati ya serikali 643 zenye akaunti za Twitter
ambazo zilitathminiwa katika nchi 161, ni mataifa 32 pekee hasa yaliyo
Afrika na Asia ya Pacific ambayo hayana shughuli nyingi kwenye Twitter.
Utafiti huo pia ulifichua kuwa mawaziri wa mataifa ya kigeni hutumia sana Twitter kutafuta ushirikiano wa kidiplomasia.
BBC
0 comments:
Post a Comment