JIJI la Dar es Salaam
lina shule za msingi na sekondari 218 ambazo zinaendelea kufundisha wanafunzi
bila kuwa na usajili kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Katibu Tawala Mkoa huo
Teresia Mbando, wakati wa kufunga kikao cha Umoja wa Walimu Wakuu wa Sekondari
(TAHOSSA) Kanda ya Dar es Salaam.
Miongoni mwa shule hizo, za sekondari 59 na za msingi 159.
"Tumezibaini shule hizi zinafundisha wanafunzi bila idhini ya Serikali na pia
kuna vituo vya chekechea 1,029 havipo rasmi, vituo vya kufundisha masomo ya
ziada 250 na hosteli 78," alisema na kuongeza;
"Vyote hivi ni bubu na ni changamoto kubwa kwa mkoa wetu
kwani ndiyo chimbuko la watoto kufanya vibaya kwenye masomo yao." Alisema
wenye vituo vya mitihani visivyo rasmi eneo la Mchikichini wana tabia ya
kuongeza alama za masomo kwa wanafunzi ili kujipatia fedha kutoka kwa wazazi
ili ionekane watoto wao wanaelewa wanachofundishwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAHOSSA Kanda ya Dar e
Salaam, Luteni Kanali Celestine Mwangasi, alisema mkutano huo ni wa pili kwa
ajili ya kubadilishana uzoefu.
Mwangasi alisema katika kikao hicho kinawakutanisha walimu wote wa
shule za serikali na kawaida pamoja na wakaguzi wa shule na watu wa Baraza la
Mitihani katika kujadili uandikishaji wanafunzi na usimamiaji mitihani na
uendeshaji.
Majira TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment