Photo 
Ni kama sikio la kufa haisikii dawa, maafisa wa Hong Kong katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Hong Kong wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya tena zilizokuwa zikisafirishwa kutokea Tanzania ambapo safari hii zilikuwa zimefichwa katikati ya kipuri cha mashine.

Dawa hizo, aina ya heroin, zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti, terehe 2 na 15 mwezi huu, zikiwa na jumla ya kilo 1.5 zenye thamani ya dola za Marekani milioni 1.3.

Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo ambapo ilikuwa vigumu kugundua hadi walipolazimika kukikata kipuri hicho kwa msumeno kubaini dawa hizo na uchunguzi bado unaendelea.

Taarifa hiyo inmefafanua kuwa kuwa adhabu ya chini kabisa ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni kifungo cha maisha au faini ya dola za kimarekani milioni 5.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top