Maandamano zaidi yamepangwa kuendelea mjini Cairo
Misri, ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi
wananuia kuandamana baada ya sala ya Ijumaa.
Haya yanajiri siku mbili baada ya maafisa wa
usalama Misri kuvunja kambi walimokua wafuasi wa Vuguvugu la Muslim
Brotherhood ambapo katika makabiliano hayo zaidi ya watu 500 waliuawa na maelfu
kujeruhiwa.
Wakati huo huo serikali ya mpito ya
Misri imemlalamikia Rais wa Marekani Barack Obama kwa kulaani mauaji ya
raia waliokuwa wakiandamana na amesitisha mazoezi ya pamoja na jeshi
la Misri ingawa hakutangaza ikiwa Marekani itasimamisha msaada
wa dola bilioni 1.3 kwa jeshi la Misri.
Kiongozi wa Mpito wa Misri amesema matamshi ya
Obama yanawapa nguvu makundi ya wanamgambo kuendelea kutekeleza vitendo
vya kigaidi.Usalama umeendelea kuimarishwa mjini Cairo, huku magari ya
kivita yakionekana kushika doria.
Muslim Brotherhood imewaomba wafuasi wake
kujitokeza kwa maandamano baada ya sala ya Ijumaa wakiitaja kama siku ya
hasira. Upande unaompinga Bw. Morsi umeomba maandamano kupinga vuguvugu
la Mosri. Kuna wito watu kulinda makanisa na makaazi nchini
Misri. Wakristo wa madhehebu ya Copt wamelengwa katika siku za karibuni.
Makanisa 25, makaazi na biashara za Wakristo
zililengwa na wafuasi wa makundi ya kiisilamu hapo Jumatano na Alhamisi.
Kuna hofu ya umwagikaji zaidi wa damu baada ya serikali kuonya kuwa polisi
watatumia risasi kujilinda na kulinda taasisi za serikali.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment