Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya makete, Francis Chaula akizungumza na wananchi katika
mkutano wa hadhara katika kijiji cha Luwumbu Makete.
Chama
cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Makete kimeishukia serikali ya
halmashauri ya wilaya hiyo kwa kumtaka mkandarasi anayekarabati maeneo
korofi katika barabara ya Bulongwa-Luwumbu kurudia kuweka kifusi imara
kwenye barabara hiyo na kutoa udongo waliouweka kwani hauna msaada
kwenye barabara hiyo.
Chama
hicho kimekwenda mbali zaidi kwa kumtaka diwani wa kata hiyo kukataa
kusaini hati ya kuidhinisha mkandarasi huyo alipwe fedha za kazi hiyo
mpaka atakaporekebisha barabara hiyo kwa kuweka kifusi imara ambacho
kitawaridhisha wananchi na watumiaji wa barabara hiyo.
Kauli
hiyo imetolewa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha
Usililo kata ya Luwumbu wilayani hapa na katibu wa CCM wilaya ya Makete
Miraji Mtaturu, ambapo pamoja na mambo mengine wananchi wameoneshwa
kukerwa na ukarabati wa barabara hiyo, ambapo kabla ya mkutano huo
msafara wa viongozi hao ulishangazwa na uwekaji wa kifusi ambacho si
rafiki wa mazingira ya kata hiyo
Kufuatia
sakata hilo, chama hicho kupitia kwa Katibu Mtaturu walimuagiza diwani
wa kata ya Bulongwa ambaye ni mjumbe wa kamati ya fedha na mipango ya
halmashauri ya wilaya ya Makete ambayo inaidhinisha malipo ikiwemo ya
wakandarasi, kupeleka taarifa wilayani kuwa mkandarasi huyo asilipwe
fedha mpaka arekebishe barabara hiyo kwa kuweka kifusi kinachokubalika
"wananchi
nawahakikishia mkandarasi huyo hatalipwa fedha, maana kifusi
alichokiweka mvua ikinyesha tu maeneo yote yatakuwa na utelezi na
hayatapitika, na huku kuna mazao na shughuli nyingi sasa hii kero hadi
lini, sisi hatutaki matusi baadaye kutoka kwa watu, tunataka kazi hii
ifanyike mara moja" alisema Mtaturu
Akihutubia
wananchi mkutanoni hapo mwenyekiti wa CCM wilaya Makete, Francis Chaula,
amewataka wananchi hao kutokubali kurudishwa nyuma kimaendeleo na
kuzitumia rasilimali zilizopo katani hapo kwa maendeleo yao wote huku
wakiwakemea na kukaa mbali na wale wanaokwamisha maendeleo yao
Amesema
kutokana na kata hiyo kupewa mfereji wa umwagiliaji ambao hivi sasa una
mgogoro na mtu aliyejitokeza na kudai eneo lililojengwa mfereji huo ni
lake na kupeleka kesi hiyo mahakamani, wapambane hadi dakika ya mwisho
kutetea mfereji huo na kwani chama hicho kipo nyuma yao kuhakikisha
wanashinda katika kutetea mradi huo wenye manufaa kwa kata hiyo
Ziara
hiyo ya viongozi wa CCM wilaya ya makete wakiongozwa na mwenyekiti
Francis Chaula imefanyika katika vijiji vya Uganga, Luwumbu, Unenamwa na
Usililo ambavyo vipo katika kata ya Luwumbu kwa lengo la kusikiliza
kero na maoni ya wananchi hao.
Via Ccmblog
0 comments:
Post a Comment