MKUU wa wilaya ya
Singida mkoani Singida, Mwalimu Queen Mlozi, amemuagiza mganga mkuu wa Manispaa
ya Singida kumuajiri kijana aliyekuwa anatumia madawa ya kulevya na kuamua
kuachana nayo.
Agizo
hilo lilitolewa na Mkuu huyo wa wilaya kufuatia ushuhuda uliotolewa na kijana
Yusufu Saimoni Shumbi mbele ya wananchi katika viwanja vya stendi kuu ya mabasi
Singida jana(juzi) katika ukaguzi wa mabanda ya Mwenge yaliyopo eneo hilo uliofanywa
na Mkuu wa wilaya.
Alisema
maelezo ya kijana huyo yanaonesha kuwa miongoni mwa kilichosababisha Yusufu
kuanza kutumia madawa ya kulevya ni kukosekana kwa kazi ya kufanya na kumpa
vishawishi vya kujiunga na makundi ya madawa ya kulevya hivyo uamuzi wa kwanza
wa serikali ni kumpa shughuli ya kufanya kijana
Alisema
vijana wanaotumia madawa ya kuelvya wako wengi na wanahitaji kuwafuatilia kwa
karibu ili kuwarejeha katika hali ya kawaida na kuokoa nguvukazi ya Taifa hivyo
Manispaa ya Singida itafute mbinu za kuwaweka karibu vijana walioko katika
janga la madawa ya kulevya waachane na madawa hayo
“Mganga
nakupa kazi moja kubwa, kuanzia leo tafuta namna ya kumpa kazi ya kufanya
kijana huyu ili asije akarejea katika madawa ya kulevya na taarifa niipate
haraka sana” alisema mkuu wa wilaya
Awali
akitoa ushuhuda wake Yusufu Saimoni Shumbi amesema alianza kutumia madawa ya
kulevya alipokuwa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Kikatiti ambako
alikuwa na rafiki zake wengine ambao walikuwa wanasoma naye na baada ya
kumaliza na kufeli mtihani aligundua kuwa alijipotezea muda shuleni
Alisema
kutokana na kutumia madawa hayo alibadilika afya yake akawa anaugua mara kwa
mara kichwa, mwili kulegea na kukosa kumbu kumbu pamoja na kukosa uwezo wa
kujimudu katika baadhi ya matendo kutokana na mwili wake kulegea mikono na
mikono
Alisema
hivi sasa ameamua kurudia mtihani wa kidato cha nne kwani awali alifanya
mtihani huo na kufeli mwaka 2011 lakini kutokana na uwezo mdogo aliokuwa nao
kutokana na kutumia madawa ya kulevya alipata daraja la nne alama 30
Kwa
upande wake mama mzazi wa Yusufu, Grace Shumbi (50) amesema mwanae ni kitinda
mimba katika familia yake ya watoto tisa ambapo wamekuwa wakiishi kwa kutegemea
kodi ya nyumba kwani alikuwa akifanya kazi ya kuhubiri neon la Mungu katika
shirika la Life Ministry na kustaafu miaka kadhaa iliyopita
Amesema
mwanae licha ya kuwa na hali hiyo amekuwa mwaminifu sana nyumbani kwani hata
ujenzi wa nyumba kubwa wanayokaa hivi sasa aliisimamia Yusufu wakati huo mama
yake akiwa anatibiwa hospitali
Amesema
hivi sasa Yusufu anamdai ada akalipe shule ili asome upya aweze kurudia mtihani
wa kidato cha nne ili aweze kuendelea na masomo kwani anaelewa kuwa ana uwezo
wa kuendelea kusoma shule na kufaulu hadi chuo kikuu bila shida ikiwa tu
atapata ada.
Via Sumia
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment