RPC Ramadhan Mungi
VIONGOZI waandamizi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Taifa akiwemo mwenyekiti wao Bw Freema Mbowe, Mbunge wa Singida Mashariki ambae ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu na mwenyeji wao mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wakamatwa na polisi mkoani Iringa
Viongozi hao wamekamatwa leo majira
ya saa 3 asubuhi kati kati ya mji wa Iringa wakati wakitokea eneo la
Kihesa kuelekea Bungeni mjini Dodoma kwa shughuli za kibunge kabla ya
jeshi la polisi kuwatia matatani na kuwafikisha kituo cha polisi .
Akithibitisha kukamatwa viongozi hao
kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa viongozi
hao walikamatwa kwa mahojiano kutokana na kutoa kauli hatarishi kwa amani
wakati wa mkutano wao uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa kwa ajili
ya mabaraza ya ukusanyaji wa maoni ni rasmu ya katiba.
Kamanda Mungi alisema kuwa kibali
ambacho Chadema walipewa kilikuwa kikianza saa 9 Alasili hadi saa 12 .;00
ila wao waliendelea na mkutano huo hadi majira ya saa 12 .25 na kila
walipofuatwa zaidi ya mara moja kuelezwa kuhusu muda wa kibali chao
kuisha bado viongozi hao waliendelea kuendesha mkutano huo huku wakitumia
vipasa sauti kutoa maneno ya dhahaka dhidi ya jeshi la polisi.
Hata hivyo alisema kuwa jeshi la
polisi lilishindwa kutumia nguvu kwa kuwakamata ama kuwashusha viongozi
hao jukwaani wakati wa mkutano huo kama njia ya kuepusha vurugu ambazo
zingeweza kutokea iwapo nguvu zingetumika kuwashusha kwa kuvunja sheria
za nchi .
"Tunawashikilia viongozi hao kutokana
na kutoa kauli hatarishi wakati wa mkutano wao wa jana (juzi)
uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa ....kwani kibali chao kilikuwa kikiisha
saa 12 .00 jioni ila wao walizidisha muda na maofisi wa polisi
waliokuwepo waliwafuata na kuwakumbusha juu ya muda waliopewa katika kibali
chao ila wao badala ya kusitisha mkutano walitumia kipasa zauti kujibu na
kutoa kauli cha hatarishi ....Jeshi la polisi lilitumia busara na kuwaacha
hadi walipomaliza na asubuhi tuliwakamata kitaalam bila ya kutokea vurugu
zozote"
Alisema kuwa viongozi hao hadi
majira ya saa 5 leo asubuhi
walikuwa wakiendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na kuwa kufikishwa ama
kutofikishwa mahakamani kutajulikana mara baada ya mahojiano hayo .
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya
Iringa Suzana Mgonakulima alisema kuwa jumla ya waliokamatwa jana ni
viongozi wanne akiwemo Mbowe, mbunge Msigwa , Lissu pamoja na diwani wa kata
ya Mvinjeni katika Manispaa ya Iringa Frank Nyalusi .
Mngonakulima alilitaka jeshi la
polisi kutimiza wajibu wake bila kutumiwa na chama chochote cha siasa
ama mtu yeyote katika shughuli zao kwani kwa kufanya hivyo ni kuondoa
imani ya polisi na wananchi.
Kuhusiana na kumamatwa na kuachiwa kwa
viongozi hoa alisema kuwa viongozi hao waliachiwa majira ya saa 5.30 asubuhi
baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya masaa matatu ambapo kila mmoja alitakiwa
kuthaminiwa na mtu mmoja kwa dhamana ya Tsh milioni 2 na wote walikidhi
masharti ya dhamana na kuruhusiwa kuendelea na safari hadi hapo
watakapotakiwa kufika polisi .
" Tunawashangaa sana polisi Iringa
Chadema kuzidisha muda dakika 5 imekuwa tatizo mbona CCM wamekuwa
wakifanya mikutano yao hadi saa 1 usiku bila viongozi wake kukamatwa
....Chadema hatuna tatizo kwa kuonewa na huu si mkutano wa kampeni ni
mkutano wa kukusanya maoni ya katiba ambao hatutapewa muda kamili na tume
...ila tunawasamehe bure polisi"alisema mwenekiti huyo wa Chadema Iringa
mjini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment