Kikosi cha Umoja wa Mataifa mashariki mwa Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo kimeanzisha uchunguzi kuhusu vifo vya waandamanaji
wawili mjini Goma.
Walioshuhudia tukio hilo waliliambia shirika la
habari la Ufaransa kwamba watu hao walikufa wakati waandamanaji
walipojaribu kuvamia kambi ya kikosi hicho karibu na uwanja wa ndege.
Waliwatuhumu askari wa Umoja wa Mataifa kutoka Uruguay kuwa walifyatua risasi dhidi ya waandamanaji.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO, bado kujibu tuhuma hizo.
Mamia ya watu waliandamana hapo jana kupinga mapigano yanayoendelea baina ya MONUSCO na wapiganaji wa M23.
Na watu kama watatu piya walikufa jana pale eneo
la makaazi lilipopigwa na mizinga - Umoja wa Mataifa unawalaumu
wapiganaji kwa hayo.
Lakini kundi la M23 limesema kamwe halikushambulia mji wa Goma.
Kiongozi wa kundi hilo, Betrard Bisimwa
akizungumza na BBC amesema kuwa hivyo ni visingizio vya kutaka jeshi la
Umoja wa Mataifa kuingilia kati.
Chanzo: BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment