Habari kutoka Mumbai, India, zinasema kuwa waokoaji
waliopiga mbizi kuwatafuta manusura hawajapata chochote. Mkuu wa jeshi
la wanamaji nchini India D. K Joshi amesema kuwa watu 18 walikuwa kwenye
nyambizi iliyozama baada ya kukumbwa na milipuko miwili mikubwa.
Waziri wa Ulinzi wa India A. K . Anthony ametaja
tukio hilo kama baya zaidi kuwahi kutokea kwa wanamaji wa nchi hiyo.
Iliwachukua wazima moto masaa kadhaa kuzima moto ambao ulionekana katika
nyambizi.
Ripoti kutoka eneo la tukio hilo zinasema kuwa
wanamaji kadhaa waliruka kutoka kwenye nyambizi kuokoa maisha yao baada
ya mlipuko. Waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali maalumu ya
wanamaji. Maafisa wakuu wa idara ya wanamaji wamesema kuwa sehemu moja
ya nyambizi hiyo ilikuwa imezama majini na eneo lingine kuchomeaka
kabisa.
Nyambizi hiyo iliyotengenezewa Urusi ilifanyiwa marekebisho miezi mitatu iliyopita kwa gharama ya Dola Miloni 8.
Chanzo: BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment