Kamishina Suleimani Kova 
Jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa   tisa   na bunduki mbili ambazo zilikutwa katika matukio tofauti ya ujambazi  jijini humo.

Mkuu wa kanda hiyo kamishina Suleimani Kova amesema kuwa miongoni mwa watuhumiwa  hao watu wawili ni raia wa nchi za Congo DRC na Uganda.

Katika hatua nyingine jeshi hilo linamshikilia  askari wa kituo cha Oysterbay ambaye yuko likizo kwa tuhuma za kutaka kuwaokoa wahalifu baada kukamatwa na raia wema eneo la Ilala jijini Dar es Salaam.

Kamishina Kova amesema askari huyo alihusika katika tukio la wizi wa dola elfu thelathini za marekani ambapo watuhumiwa baada ya kuwekwa chini ya ulinzi alitaka kuwachukua kwa lengo la kuwatorosha badala ya kuwapeleka kituo cha polisi.

Aidha baadhi ya watuhumiwa hao walikutwa na sare za jeshi la wananchi JWTZ,sare za polisi,risasi pingu na funguo zake vitu ambavyo vinadaiwa kutumika kuwalaghai na kuwatisha wananchi wakati wakifanya matukio ya uhalifu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top