Rais wa Marekani, Barack Obama
Marekani imeachana na jitihada za kutafuta uungwaji
mkono wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuichukulia hatua Syria
kwa utumiaji silaha za kemikali.
Hii ni kufuatia Urusi kupinga rasimu ya maazimio yaliowasilishwa kwenye mkutano wa wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo la usalama.
Akiilaumu Urusi kwa uamzi wake alisema msimamo wa nchi hiyo wa
kutobadili maoni kwa chochote, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni,
Maria Harf amesema kuwa Marekani haitaruhusu alichotaja kama uzembe wa
kidiplomasia kutumiwa kama ngao ya kutetea Serikali ya Syria.
Azimio
lilioandikwa na Uingereza lingaliruhusu hatua za kuwalinda raia wa Syria
lakini likapingwa na Urusi katika kikao cha wanachama watano wa kudumu
katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Urusi, ambayo hutoa silaha kwa Serikali ya Syria
na pia mshirika wake mkuu kimataifa, ilisema kuwa kura ya azimio hilo
inapaswa kuahirishwa hadi tume maalumu ya umoja wa mataifa ya kuchunguza
matumizi ya silaha za kemikali nchini humo itakapokamilisha kazi yake.
Msemaji huyo alielezea hali ya Marekani ya
kutoridhika na hali ya upole inayoendelea katika Umoja wa Mataifa, na
akasisitiza kwamba kwa wakati huu Marekani haioni matumaini yoyote ya
kuungwa mkono na Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa na kwa sasa
itatilia mkazo mashauriano na mataifa mengine washirika kabla ya
kuchukua hatua yoyote inayofaa hivi karibuni.
Alisema kuwa hadi kufikia sasa Rais Obama
hajafanya uamuzi wowote juu ya hatua inayopaswa kuchukuliwa, lakini
akaongeza kuwa ni dhahiri kuwa silaha za kemikali zilitumiwa nchini
Syria na kwamba wa kulaumiwa ni utawala wa Rais Assad.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment