Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa idara ya
uhamiaji bwana Abasi Mussa Irovya amesema hatua kali za kisheria zitachukulia
kwa mwananchi yeyote ambaye atahusika kuwahifadhi wahamiaji hao.
Bwana Irovya ameongeza kuwa kwa sasa idara ya uhamiaji ipo
macho katika kuhakikisha hakuna muhamiaji anayetoka sehemu moja kwenda nyingine
kwa lengo lakuukimbia mkono wa sheria.
Aidha msemaji huyo amewataka wahamiaji haramu kuhakikisha
wanaitumia fursa iliyotolewa na serikali ya kuondoka haraka nchini kabla
hawajakutana na operesheni hiyo yenye lengo la kuwarudisha wahamiaji haramu
katika nchi zao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment