Watanzania wametakiwa kuwa waadilifu na wazalendo kama ambavyo viongozi waliotangulia na kuliletea bara la Afrika Uhuru walivyofanya watangulizi wa  bara la Afrika mafanikio katika harakati za uhuru.

Hayo yamesemwa aliyewahi kuwa kiongozi wa serikali na CCM Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika mahojiano maalum kuhusiana na kumbukumbu ya miaka 95 tangu kuzaliwa kwa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Madiba Mandela.

Mzee Kingunge amesema Mandela wakati wa uongozi wake alipigania haki kwa ajili ya manufaa ya taifa na wananchi wake hali iliyomjengea heshima kubwa barani Afrika na Ulimwenguni kote.

Mzee Kingunge amewataka vijana kujifunza kuwa wazalendo kupitia historia ya Mzee Mandela ambaye alianza kupigania harakati za ukombozi tangu alipokuwa kijana mdogo na kufanikiwa katika vita vya ubaguzi wa rangi nchini humo.

Mzee Nelson Madiba Mandela anaadhimisha miaka 95 akiwa hospitalini jijini Pretoria ambapo alikuwa rais mweusi wa kwanza kuliongoza taifa la Afrika Kusini mara baada ya kukomeshwa kwa ubaguzi wa Rangi nchini humo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top