Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema Tanzania sio mali ya
chama chochote cha siasa wala kundi lolote la watu wakati akihojiwa
katika kipindi cha Makutano na Fina Mango.
Mheshimiwa Peter Msigwa alitoa kauli hiyo alipoulizwa anaonaje mwamko wa kufanya mabadiliko unaoendelea ikiwemo mchakato wa katiba mpya.
Aliwalaumu watu wa kipato cha kati kwa kusema wao ndio kikwazo cha maendeleo kwa sababu ya kuridhika na vitu vidogo walivyovipata, "Kila mtu aingie acheze huu mchezo kwamba ni wakati uliofika wa kuibadilisha Tanzania, tuibadilishe kifikra".
"Watu wengi mmekaa maofisini na kompyuta zenu na vijumba vidogo mmejenga na vigari vidogo mmeweka nje mnaogopa, lakini kama tutaendelea kuruhusu akili ndogo iendelee kutawala hatutaenda popote" alisema Mheshimiwa Msigwa.
Hata hivyo aliipongeza tume ya katiba kwa kusema ameridhishwa na ilivyofanya kazi yake kutokana na hofu waliyokuwa nayo baada ya mchakato wa kuandaa katiba mpya ambao ulianzishwa na CHADEMA kuchukukuliwa na kugeuzwa agenda ya chama tawala na hivyo kuleta wasiwasi wa haki isingetendeka hasa ile ya uwakilishi katika utoaji maoni ya katiba.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment