Na Jennifer Chamila, MAELEZO
Msajili
wa vyama vya Siasa nchini amewaasa wanachama na viongozi wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutumia muda wao kufanya shughuli za
siasa ili kuchangia maendeleo ya nchi badala ya kutumia uwezo na muda
wao kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na kuhatarisha amani ya nchi.
Pia amepinga tamko la chama hicho la kuanzisha mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchi nzima.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es
Salaam na kusainiwa kwa niaba ya Msajili wa vyama vya siasa Sisty
Nyahoza alisema kuwa hajawahi kuruhusu CHADEMA au chama chochote cha
siasa kufanya mafunzo ya ukakamavu au mafunzo ya kutumia nguvu ya aina
yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote yule.
Anaongeza
kuwa CHADEMA wanaruhusiwa kuanzisha vikundi vya kujilinda lakini
hawaruhusiwi kuanzisha mafunzo ya kutumia nguvu kwaajili ya kujilinda
kama walivyotangaza katika mikutano yao ya hadhara kwani ni kinyume na
Demokrasia na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano.
Nyahozo
ametoa ufafanuzi kuhusu vikundi vya ulinzi na usalama vilivyopo katika
Katiba ya Vyama vya Siasa kwamba vikundi hivyo haviruhusiwi kufanya
mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote katika kutekeleza majukumu yao.
Bali
wajibu wao ni kutoa taarifa wa vyombo vya Dola pale wanapo sikia au
kuona uhalifu ukitokea na wala sio kupambana na wahalifu au watu
wanaotaka kuwadhuru kama tamko la CHADEMA la tarehe 9 mwezi huu linavyo
sema.
"Hakuna
maelezo yoyote katika Katiba ya CHADEMA yanayoruhusu kutumia nguvu
kufanikisha shughuli za kulinda mali na Viongozi wa Chama. Ni vyema
wananchi wote waelewe kuwa Sheria za Nchi zimeweka masharti maalumu kwa
Vyama Vya Siasa kutokana na umuhimu wa vyama hivi katika kudumisha aman
utulivu na umoja wa Kitaifa", alisema Nyahoza.
Alisema
kuwa kutokana na Ibara ya20(2)C ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1997 inasema kuwa "Bila kujali masharti ya ibara ya
(1) na (4),haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kuandikishwa
ambapo kutokana na katiba au sera yake:-kinakubali au kunapigani
matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya
kisiasa.
Nyahoza
alimaliza kwa kuwataka CHADEMA kuacha kutekeleza mpango walio tangaza wa
kuanzisha makambi ya kufanya mafunzo ya kujilinda kwa vijana wao nchi
nzima,kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi na endapo
watashindwa kutii agizo hilo hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mwisho.
Via Mjengwablog
0 comments:
Post a Comment