Vijana hawa wanaungwa mkono na jeshi na hata wamepewa mafunzo kukabiliana na Boko Haram.
Takriban watu 20 wameuawa nchini Nigeria baada ya
makabiliano makali kati ya makundi ya vijana waliojihami na wapiganaji
wa kiisilamu.
Hii ni kwa mujibu wa jeshi na vijana wanaotoa ulinzi kwa wanavijiji.
Kulingana na vijana hao wanaotoa
ulinzi kwa niaba ya serikali, wapiganaji walivamia kijiji cha Dawashe
kaskazini mwa nchi siku ya Jumamosi , kukabiliana na wapiganaji hao wa
kiisilamu ambao nao walilipiza kisisasi kwa kutumia silaha nzito huku
wakiwaua raia.
Kikundi hicho cha ulinzi kiliibuka mwezi Mei na kuanza harakati zake wakati huo.
Kimeahidi kusaidia serikali kupambana na wapiganaji wa Boko Haram.
Zaidi ya watu 2,000 wameuawa tangu mgogoro huu kuanza mwaka 2009.
Kundi la Boko Haram linasema kuwa linapigana dhidi ya serikali kutaka kuwa na utawala wa kiisilamu kote Nigeria.
Jeshi linatizama wapiganaji hao kama washirika
wake na hivyo limewapa mafunzo kulisaidia katika harakati dhidi ya
wapiganaji hao wa kiisialamu.
Kiongozi wa vijana hao Aliko Musa alisema kuwa
watu 25 waliuawa mjini Dawashe katika jimbo la Borno ambalo ndilo kitovu
cha harakati za Boko Haram.
Naye msemaji wa jeshi Haruna Mohammed Sani alithibitisha kuwa watu 20 waliuawa.
Chanzo: BBCswahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment