Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa.
Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa, amesema uamuzi wa kuvifuta vyama hivyo unaweza kuwa na athari kubwa kwani utahitaji gharama kubwa za kufanyika uchaguzi jambo ambalo sio la kukimbilia.
Msajili huyo alipotakiwa kuelezea juu ya ofisi yake kuvifuta vyama hivyo viwili vya CCM na CHADEMA alisema ofisi yake ina mamlaka hayo ila hiyo ni hatua ya mwisho kuchukuliwa iwapo itabidi.
Alisema ofisi yake inahitaji kukutana na vyama hivyo kwani ndio njia sahihi ya kufikia muafaka kwa maslahi ya vyama hivyo na wananchi kwa ujumla.
“Ni lazima jamii ikatambua kuwa maamuzi haya yanahusu CCM ambayo ipo madarakani ambapo matokeo yake ni kuvunja Serikali na kwa CHADEMA ni kuwaondoa wabunge wake hivyo uchaguzi kufanyika tena,
Kauli hiyo imetolewa na Msajili wa vyama vya siasa ikiwa ni siku chache baada ya kutokea kwa mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni ya udiwani uliokuwa unaendeshwa na CHADEMA katika viwanja vya Soweto mjini Arusha kabla ya Polisi kuibuka tena jumanne mapema wiki hii kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa katika uwanja huo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment