Waziri wa fedha Kosti Manibe anachunguzwa kwa madai ya ufisadi.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, amewafuta kazi mawaziri wawili serikalini wanaohusishwa na kashifa ya ubadhilifu wa mamilioni ya dola .
Bwana Kiir pia amewaondolea kinga dhidi yao wakiwa waziri wa fedha
Kosti Manibe na mwenzake anayehusika na maswala ya baraza la mawaziri
Deng Alor kushtakiwa na kuamuru kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi yao wawili hao wangali kutoa kauli yoyote kuhusu tuhuma hizo.
Wadadisi wanasema kuwa ufisadi ni moja ya
vikwazo vikubwa kwa utawala wa Kiir , Sudan Kusini tangu nchi hiyo
kujitawala mwaka 2011, na kulifanya kuwa taifa changa zaidi duniani.
Mwezi juni, Bunge la Sudan Kusini lilipiga kura
kuwasimamisha kazi kwa muda maafisa wakuu 75 wa serikali waliohusishwa
na ufisadi.
Rais Salva Kiir alituma ujumbe kwa maafisa wa
iliyokuwa serikali ya zamani ikiwataka warejeshe dola bilioni 4 pesa
walizodaiwa kuiba.
Hata hivyo serikali ilitangaza kwenye mtandao wake rasmi kuwa bwana Manibe na bwana Alor, wataachishwa majukumu yao mara moja.
Rais Kiir aidha aliwaamuru kufika mbele ya
kamati inayochunguza kashfa hiyo kujibu maswali kuhusu kuhusika kwao na
sakata ya mamilioni ya dola pesa za serikali.
Pesa hizo zilidaiwa kutumika kununua kabati
maalum za kuweka pesa ambazo haziwezi kuteketea , lakini haijulikani
ikiwa kweli waliweza kuzipokea.
Sudan Kusini ina utajiri wa mafuta , lakini ni
moja ya nchi barani Afrika ambazo zina miundo mbinu duni na taasisi duni
za kiafya na elimu ilijipatia uhuru kutoka kwa Sudan mwaka 2011 mwezi Julai baada ya vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment