SERIKALI HAIJAFUTA MITITIHANI YA TAIFA YA MASOMO YA DINI
Serikali inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa haijafuta Mitihani ya Taifa ya masomo ya Dini kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari. Masomo hayo ni pamoja na Elimu ya Dini ya Kiislam, Bible Knowledge, Islamic Knowledge na Divinity.
Masomo ya Dini yanaendelea kufundishwa shuleni na kutahiniwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Hata hivyo, Serikali inakusanya maoni kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa Mitihani ya Dini.
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI 01/06/2013
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment