Wana JF,
Kwanza namshukuru Mungu kwa kutupa fursa ya kuishi tena (2nd chance) mimi na mdogo wangu. Mungu yu mwema kwetu.

Katika ajali hii, huwezi kutarajia kuwa tumetoka tukiwa hai na tunaendelea vema kama tulivyo sasa.

Aidha, nawashukuru wote waliotoa pole zao kwetu via JF na kututakia kupona haraka. Tunashukuru sana na tunazidi kufarijika kwa ushirikiano wenu katika maombi (na baadhi walituma michango itusaidie katika matibabu). Moderators, shukrani kwa kuendelea kulisimamia jukwaa hili kwa weledi mkubwa.

Napenda kuwashukuru wanasiasa watatu; ndugu Zitto Kabwe, Dr. Faustine Ndugulile na Ndugu Hussein 
Bashe - ambao wameonyesha kujali tangu tunapata ajali hadi sasa (wanatujulia hali tunavyoendelea); hii inatia moyo na kuonyesha kujali kwao kwetu. Mungu awazidishie muendelee kuwa na moyo huu.

Shukrani zetu ziende kwa wana JF wa Nzega, Mwanza na Dar; ambao wamekuwa nasi bega kwa bega tangu siku ya ajali. Ni wengi lakini inakuwa vigumu kuwataja kwenye shukrani zetu hizi bali tunapenda wafahamu kuwa tunawashukuru sana.

Tunawashukuru sana wengine wote ambao kwa njia tofauti wamekuwa wakitaka kujua tunaendeleaje kiafya na kuwajuza hapa; kutokana na mazingira tulikuwa tunashindwa kuwajibu wote lakini wengi tumewajibu kuwafahamisha kilichotokea na tunavyoendelea.

Ndugu zangu, tupo hai kwa mapenzi ya Mungu tu!

Nini kilitokea?
Inakuwa vigumu kuelezea kwa kirefu kilichotokea. Kuwa ni mwendo kasi? Sijui. Kuwa ni mkono wa mtu? Pia sijui. Kuwa ni bahati mbaya? Naweza kusema hivyo! Hatumlaumu yeyote katika hili na hatumnyooshei kidole yeyote. Kwa dereva yeyote anafahamu nini kinaweza kutokea pale 'Sterling Rod' inapokatika ukiwa katika mwendo zaidi ya spidi 80.

Yapo mengi yanaweza kuhisiwa, yapo mengi yanaweza kusemwa lakini ambacho tunaweza kukiri ni kuwa Mungu yu mwema kwetu.

Hali yetu:
Baada ya ajali, mdogo wangu ambaye pia ni member wa JF kama Chachu Ombara, alibainika kuvunjika mfupa wa kati ya kiwiko na bega mkono wa kushoto na sasa amefanyiwa upasuaji na madaktari bingwa Muhimbili, anaendelea vema.

Binafsi nilibainika kuwa na uvimbe kidogo kwenye ubongo upande wa kulia; naendelea vema namshukuru Mungu.

Mwisho:
Ushauri wangu kwa wanaoendesha magari, wasafiri kwenye ruti ndefu na hata katika hali ya kawaida:
- Kabla ya safari yoyote mwite Mungu na ujikabidhi kwake, atakuitikia kwa namna ya kipekee
- Unapoendesha, funga mkanda. Hata kama umekaa siti ya nyuma (katika gari binafsi).
- Ukiwa barabarani (dereva), jitahidi kuzingatia alama za barabarani; wajali madereva wengine kama ambavyo ungependa wakujali.

Nasikitika kuwa huenda nisijibu maswali ambayo labda yanaweza kujitokeza kutokana na kuwa nina matatizo ya kuumwa kichwa (kilijigonga sana chini wakati gari linapinduka) lakini naamini nikikaa vema nitarejea na aidha kujibu au nikiwa nimechelewa nitatuma PM kwa mhusika.

Asanteni sana.

Maxence

===================

Tokana na maoni ya wengi wa wadau wa Jukwaa La Siasa kutokua na taarifa hii mbaya ya Ajali ilipokua imetangazwa hapa, mtuwie radhi Moderators kwa maamuzi ya kuhamishia habari hii Jukwaa La Siasa toka habari na hoja Mchanganyiko.

Habari hiyo ya ajali ilipostiwa hapa na inapatikana kwenye kiunganisho hiki kilicho ambatanishwa -Maxence Melo apata Ajali mbaya Maeneo ya Nzega.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/06/maxence- melo-awashukuru-watanzania.html#ixzz2V8rWXi5Y
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top