Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said
Mwema.
JESHI la Polisi, limeendelea kukumbwa na kashfa nzito, baada ya askari
wake Sajenti Maichael mkoani Mara, kukutwa na risasi 200 ambazo
haijulikani alitaka kuzipeleka wapi.
Askari huyo, alitiwa mbaroni na askari wenzake wa kikosi cha intelejensia.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya jeshi hilo, ziliiambia MTANZANIA mjini Musoma jana, kuwa askari huyo (jina linahifadhiwa) kwa sababu za kiuchunguzi alikamatwa Juni 3, mwaka huu saa 11 alfajiri, akiwa ndani ya basi la Kampuni ya Mohamed Trans linalofanya safari zake kati ya Musoma na Dar es Salaam.
Askari huyo, ambaye yupo kwenye Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), inaelezwa ni mtunza ghala la silaha.
Habari zinasema amekuwa akituhumiwa mara nyingi, kuchukua silaha na kuwaazimisha watu ambao huenda kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali.
Habari zinasema kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema ametengeua likizo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Asalom Mwakyoma.
Tayari Kamanda Mwakyoma alikuwa njiani kuelekea kijijini kwao, kwa ajili ya mapumziko.
Akizungumza na MTANZANIA, Mnadhimu wa Jeshi hilo mkoani Mara, Rashid Mohamed ambaye amekaimu nafasi ya Kamanda alikiri kuwapo kwa tukio hilo na bado wanaendelea kulifanyia kazi.
"Ni kweli kama ulivyosikia taarifa hizi, lakini bado tunazifanyia kazi kwa undani ili kuweza kubaini kwa nini askari huyo alikuwa na risasi hizo na pale tutakapokamilisha mtapata taarifa kamili, naomba mtuache kwanza.
Pamoja na jeshi hilo, kuwa na usiri mkubwa wa tukio hilo, baadhi ya askari waliiambia MTANZANIA tukio hilo lipo.
Kwa muda sasa, jeshi la polisi limekuwa likipoteza mwelekeo kutokana na askari wake kujihusisha na vitendo viovu.
Miongoni mwa vitendo hivyo, ni pamoja na askari kushiriki kusafirisha gunia 18 za bangi, kubambikizia mfanyabiashara kesi ya mauaji wilayani Kilosa, kushiriki ujambazi na kupora Sh milioni 150 katika eneo la Kariakoo mjini Dar es Salaam.
MISUNGWI
Katika hatua nyingine, habari kutoka Misungwi mkoani Mwanza, zinasema askari Polisi mmoja wa Kituo cha Misungwi, amevamia shule maalum ya walemavu wa ngozi (albino) na mtindio wa ubongo akiwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), kwa nia ya kumsaka mlezi wa wanafunzi hao, Judith Mlolwa na kuzua taftrani kubwa.
Askari huyo, ambaye alionekana kuwa na hasira kwa kile kinachodaiwa kumsaka Mlolwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Misungwi, alisababisha taharuki kubwa ya watoto kukimbia ovyo na kuumia vibaya.
Tukio hilo, lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, saa 2 usiku shuleni hapo, ambapo askari huyo aliyefahamika kwa jina la Faraji mwenye namba G.3408 alipoamua kutumia nguvu kuingia shuleni hapo.
Katika purukushani hizo, askari huyo alimjeruhi mlinzi wa shule hiyo, Nyamizi Katemi kwa kutumia kitako cha bunduki na kumng’oa meno matatu.
Baada ya askari huyo kujibiwa hivyo, aliingia ndani ya uzio wa shule na kuanza kuwafukuza ovyo ovyo, pasipo na sababu za msingi.
Kutokana na Katemi kumsihi askari huyo, lakini hakumsikiliza ndipo alianza kumshambulia.
Naye, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Kulwa Ng’welo, alisema jana kuwa baada ya kuona vurugu hizo, alipiga simu polisi na askari wawili walifika shuleni hapo na kushindwa kumdhibiti askari mwenzao ambaye wakati huo tayari alikuwa akitamba na kudai kuwa lazima atimize dhamira yake.
Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alipotakiwa kuelezea tukio hilo, alisema hajapata taarifa na aliahidi kulifuatilia.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment