Taarifa
zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne
wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani
wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni
hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa
masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta
wakivamiwa na watu wanne na kuamriwa watoe komputa zao na pochi za
fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi
hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha, na majambazi
kuanza safari yao.
Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu
vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi
tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na
kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.
Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na
uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini
ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo walipoamua kujikusanya
na kuamua kuwafuata viongozi.
Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa
Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote
iliyotoka, ingawa FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia suala hilo ili
kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.
Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar es salaam na
kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya kikatili
chuoni hapo. Endelea kufuatilia katika mtandao huu amboa umefunga safari
ya kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia nini kinaendelea.
Mbali na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi wa hadharani katika shule za
Chuo hicho ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa wakiporwa komputa
zao mchana kweupe maeneo ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya uandishi wa
Habari na Mawasilinao ya Umma (SJMC).
Suala lizi limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.
Chanzo: The Choice
0 comments:
Post a Comment