Na Anna Nkinda – Yokohama
Watumiaji wa lugha ya Kiswahili wamezidi kuongezeka nchini Japani hadi kufikia hatua ya kuwa na mshindano kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Soka kilichopo nchini humo.
Watumiaji wa lugha ya Kiswahili wamezidi kuongezeka nchini Japani hadi kufikia hatua ya kuwa na mshindano kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Soka kilichopo nchini humo.
Hayo
yalisemwa hivi karibuni na Prof. wa chuo hicho Midori Uno wakati akiongea na Mke
wa Rais mama Salma Kikwete alipokutana naye katika hoteli ya
Intercontinental mjini Yokohama.
Prof.
Uno ambaye ni Mwalimu wa kiswahili katika chuo hicho alisema kuwa hivi
Sasa wananchi wengi wa Japani wana kiu ya kujifunza na kuzungumza
lugha ya Kiswahili kwani ni rahisi kueleweka.
“Katika
jitihada zangu za kuwafanya Wajapani wengi wajue lugha ya Kiswahili
nimetengeneza kamusi ya maneno ya Kijapani kuwa ya Kiswahili ambayo
watu wengi wanaitumia kwa sasa kwani wengi wajapani wengi wanapenda
kujifunza lugha hii”, alisema Prof. Uno.
Mashindano hayo ya lugha ya
Kiswahili ambayo hufanyika mwezi wa kumi na moja kila mwaka huwa ni ya
kuandika na kusoma hotuba ambapo mshindi wa kwanza anapewa cheti, tuzo
ya muanzilishi wa chuo hicho, vikombe na zawadi mbalimbali.
Kwa
upande wake Mke wa Rais mama Salma Kikwete alimpongeza Profesa huyo kwa
jitihada zake za kukuza lugha ya Kiswahili nchini humo na kumuomba
aendelee zaidi kufanya hivyo.
Alisema
kuwa watanzania wana vitu vyao vya kujivunia kama Taifa, moja ya vitu
hivyo ni lugha ya Kiswahili ambayo imewaunganisha watanzania wote na
kuwa kitu kimoja ndani na nje ya nchi.
Mama
Kikwete alisema, “Ili kumfikia mtu mmoja au watu wengi zaidi ni lazima
kuwe na lugha ya mawasiliano hivyo basi nasi tunatumia lugha hii
ambayo iliwaunganisha watanzania wote wakaweza kupigania uhuru wa nchi
yao kipindi cha mkoloni”.
Alisema
kuwa lugha ya Kiswahili inaongelewa maeneo mengi ya Afrika ya Mashariki
na ndani ya Bara la Afrika na hivi sasa viongozi wa Umoja wa Nchi za
Afrika (AU) waliikubali lugha hiyo kuwa lugha ya mawasiliano .
Profesa
Uno alikuja nchini kabla ya kupata uhuru kwa ajili ya kufanya kazi za
kujitolea na aliporudi nchini kwake aliamua kuwafundisha wajapani lugha
ya Kiswahili pia nchini humo redio Japani (NHK) iliyoanzishwa mwaka 1964 inatangaza matangazo
yake kwa lugha ya Kiswahil.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment