Waziri Mkuu, Mizengo pinda akitokwa na machozi kutetea wanyonge

Jana waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alitoa onyo kali kwa watu wanokaidi maelekezo ya dola na ili kusisitika kauli yake akasema polisi watazidi kutoa adhabu kali kwa wananchi wanaohatarisha amani ya nchi.

Kauli hiyo aliitoa Bungeni jana kufuatia vurugu zilizotokea wakati wananchi na wana-CHADEMA walikuwa wamekusanyika Viwanja vya Soweto Arusha kwa lengo la kuaga miili ya waliokufa katika mabomu yaliyolipuliwa tarehe 15.06.2013 ambapo jeshi la polisi lililazimika kutumia mabomu ya machozi na kuwatia mbaroni wabunge wanne wa CHADEMA kwa kosa la kukusanyika kinyume na utaratibu.

Kauli ya Pinda inaonekana kuruhusu matumizi ya nguvu kubwa zaidi kukabiliana na wananchi ingawa anajua fika kuwa zinaweza kusababisha maafa.

Kauli kama hizi sio mara ya kwanza kutoa Bungeni kwani mwaka 2009 aliwahi kutoa kauli kuwa watu wanaoua albino wauawe. 

Tofauti ni kuwa wakati mwaka 2009 alikuwa akitetea wanyonge dhidi ya wauaji na waliowasababishia vilema watu wasio na hatia, kauli ya jana inaruhusu matumizi ya nguvu kupita kiasi ambayo mwisho wake ni maafa kwa watu wasio na hatia.

Tofauti nyingine ni kuwa wakati 2009 alitoa machozi kupigania wanyonge, jana hakufanikiwa kufanya hivyo Mtoto wa mkulima.
 
Jikumbushe  kisa cha 2009 ilivyokuwa.Waziri Mkuu alifikia hali hiyo wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Hamad Rashid Mohamed, aliyemtaka aeleze sababu zilizomfanya atoe kauli ya watu wanaowaua maalbino nao pia wauawe. 
Pinda alitoa kauli hiyo hivi karibuni akiwa ziarani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Juzi, kambi hiyo ilitoa tamko mbele ya waandishi wa habari ikimtaka Waziri Mkuu aachie ngazi kutokana na kauli hiyo kwa madai kwamba inapingana na utawala bora wa kisheria. 
Baada ya kupewa nafasi na Spika, Samuel Sitta, kuuliza swali la nyongeza, Kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni alipomuuliza swali lililomfanya Waziri Mkuu ashindwe kuvumilia kutoa machozi wakati akielezea adha wanazozipata maalbino. 
``Kwa mtu ambaye hajapata nafasi ya kukutana nao (maalbino) na wakamueleza wanayoyapata…(sauti yake ikabadilika ghafla na kutokwa na machozi), wauaji hawa hawawezi kuvumiliwa. Katika mazingira kama haya, Watanzania hatutakuwa tayari kuwavumilia wauaji hao,`` alisema kwa sauti ya huruma.
Picha na habari kwa Hisani ya IPPMEDIA
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top