Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, akiwa amelazwa kwenye ndege
akifungwa mkanda tayari kwa kusafirishwa kutoka Arusha na kuhamishiwa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, amehamishiwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi, baada ya kuumizwa
kwenye vurugu zilizotokea Kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli, Arusha.
Akizungumza mjini hapa jana, Nassari alisema ofisi
ya Bunge ndiyo imeamua kumhamishia Muhimbili kutokana na majadiliano na
madaktari waliokuwa wakimhudumia Hospitali ya Arusha ya Lutheran
Medical Center alipokuwa amelazwa.
“Bunge limegharamia kunisafirisha hadi Muhimbili
kwa matibabu zaidi, ofisi ya Bunge ndiyo imetafuta ndege ndogo ya
kunipeleka,” alisema Nassari.
Alisema hadi jana alikuwa anasumbuliwa na maumivu
ya mgongo na nyuma ya shingo, ambako alipigwa rungu na vijana wa Kimasai
(Morani) na wafuasi wanaodaiwa kuwa wa CCM.
“Baada ya kunipiga nilifanikiwa kutoroka hadi eneo
la Minjingu kunusuru maisha yangu, baadaye ilibidi nitafutiwe pikipiki
hadi eneo la barabara kuu ndipo niliwakuta askari wa usalama barabarani,
waliniombea usafiri hadi hospitali,” alisema Nassari.
Hali tete ya usalama
Katika hatua nyingine, Nassari alieleza
kusikitishwa na hatua ya kutaka kuchukuliwa kwa mahojiano mmoja wa
majeruhi, ambaye alieleza alimuona mtu aliyetupa bomu kwenye mkutano wa
kampeni wa Chadema Juni 15 Uwanja wa Soweto.
“Walikuja polisi kama sita hivi wakimtaka huyu
majeruhi, hali ambayo ilizua malumbano hadi nilipongilia kati na
nikalazimika kulala naye karibu ili wasimchukue,” alisema Nassari.
Chadema wasafirisha maiti mbili
Licha ya juzi kutokea tafrani ya mabomu Uwanja wa
Soweto na kushindwa kuagwa marehemu, watatu waliofariki kutokana na
mlipuko wa bomu.
Hata hivyo, Chadema kilifanikiwa kusafirisha maiti
mbili; Ramadhan Juma(15) mkazi wa Tabora na Amir Ally(7), mkazi wa
Lushoto, mkoani Tanga.
Marehemu Judith Moshi (25)ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bawacha Kata ya Sokone 1, anatarajiwa kuzikwa leo.
Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment