Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia viongozi wanne wa CHADEMA na watu wengine 60 huku likiendelea kuwatafuta wabunge wawili  wa chama hicho na watu wengine.

Kamishina wa Operesheni wa Mafunzo wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, amesema licha ya watu hao kukamatwa pia wamekamata pikipiki 106 na baiskeli 16 ambazo zilitelekezwa.

Chagonja amesema limewatia nguvuni watu hao kwa makosa ya kuhutubia mkutano haramu wakati wa kuwaaga marehemu waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa bomu uliotokea katika eneo la Soweto jijini humo mwishoni mwa wiki.

Makosa mengine ni wanayotuhumiwa kwayo ni kufunga barabara na kuwashambulia askari polisi.

Amesema wataendelea kubaki korokoroni hadi uchunguzi utakapokamilika.

Chagonja amewataja Wabunge waliotiwa nguvuni kuwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunai (Mbulu) Said Arfi (Mpanda Mjini) na Joyce Nkya (Viti Maalum).

Wanaotafutwa ni pamoja na Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambao waliponyoka mikono ya polisi.

Wakati huo huo, habari nyingine zinasema Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) amepata ajali katika eneo la Kasheki, Hanang' baada ya gari lake kugonjana na basi la abiria na kuharibika vibaya, alipokuwa njiani kuelekea Arusha ili kuungana na wabunge wenziye katika shughuli ya kuwaaga marehemu wa mlipuko wa bomu hilo la Soweto, Arusha.

Inaarifiwa kuwa hakuna aliyejeruhiwa katika ajali hiyo.

Chanzo:Wavuti
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

1 comments:

Unknown said... June 18, 2013 at 10:27 PM

hawa sio polisi, ila ni fisi wala watu.

 
Top