Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mazungumzo na mwenyekiti wa makampuni ya VIRGIN ya Uingereza Bwana Richard  Branson  kwa nia ya kumshawishi ili  kuwekeza Tanzania katika masuala ya anga.

Bwana  Branson ameahidi kulifanyia utafiti suala hilo ili kampuni yake ya Virgin Atlantic Airways kuwekeza katika masuala ya ya anga na na usafiri wa njia ya reli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, alikuwa miongoni mwa viongozi hao wachache wa Afrika waliokutana na Waziri Mkuu Cameron ambaye pia ametaka Serikali za nchi zinazoendelea kuonyesha uwajibikaji mkubwa zaidi na uwazi zaidi katika matumizi na mapato ya kodi yanayotokana na maliasili hizo.
 
Katika mpango huo, Uingereza inataka kuzishawishi nchi za G8 kusaidia nchi zinazoendelea kujenga uwezo wa kutambua mali asili zilizopo, kutambua thamani yake, kodi inayolipwa na kama inastahili na kuzitaka kampuni zinazowekeza kuwa wazi zaidi katika biashara zao na shughuli wanazofanya  ili nchi na watu wake ziweze kufaidika na mali asili yake.

Nchi wanachama wa G8 ni Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan,Urusi, Marekani na Uingereza
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top