Jumamosi ya Juni 15, 2013 Jiji la Arusha kwa mara ya pili ndani ya kipindi kifupi liliendelea kuandika historia ya hatari kwa kutokewa na vitendo vya kigaidi. Vitendo vya kurusha mabomu kwenye mikusanyiko ya watu na kusababisha maafa.
Tukio la kwanza lilitokea Mei 5, 2013, katika
Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na
kusababisha vifo vya watu watatu. Tukio hilo kwa sasa kesi yake iko
mahakamani.
Hata hivyo tukio la Jumamosi iliyopita lilitokea
kwenye Uwanja wa Soweto mjini Arusha wakati wa mkutano wa kukamilisha
kampeni za udiwani wa Chadema. Wasiwasi mkubwa ulizuka katika tukio hilo
ni kuhusishwa polisi na vifo vilivyotokea.
Kubwa zaidi ni kifo cha mtoto Amir Ally (7)
anayedaiwa kupigwa risasi na polisi. Maelezo ya kifo cha Ally
yamenukuliwa kutoka kwa mtoto mwenzake Abubakar Adam (11), ambaye
amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru akiuguza majeraha yanayodaiwa
kutokana na risasi.
Licha ya hao wawili, Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali
ya Arusha Medical Lutheran Center (ALMC), Dk Paul Kisanga aliwataja
watoto wengine wawili ndugu Fatuma na Sharifa Jumanne ambao wamepelekwa
Nairobi, Kenya, kwa matibabu zaidi baada ya miili yao kukutwa na vyuma.
Dk Kisanga alimtaja mtoto mwingine Fahad Jamal (7)
ambaye yuko chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU),
akisubiri timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Kwa mujibu wa Dk Kisanga watoto hao watano
walipatwa na matatizo hayo wakati wakitoka madrasa eneo la Kaloleni
(Madrasa ni shule zinatoa elimu ya dini ya Kiislamu), iliyopo jirani na
Uwanja wa Soweto.
Tukio la Soweto limekuwa na matukio mawili ndani
yake; kwanza ni tukio la kurushwa bomu ambalo mtuhumiwa wake
hajafahamika, tukio la pili ni matumizi ya silaha za moto ambazo sababu
za matumizi yake na wahusika bado ni kitendawili.
Hata hivyo, mashuhuda wa tukio hilo akiwamo mtoto
Amir Ally wanadai polisi walipiga risasi watu, wengine wanakwenda mbali
zaidi kwa kudai kuwa mtuhumiwa wa bomu hilo alionekana akisafirishwa na
gari pale wananchi walipotaka kumvamia.
Wakuu wa polisi kwa upande wao wamekiri kupatikana
kwa maganda ya risasi katika eneo la tukio, hii ina maanisha kwamba ni
kweli ndani ya tukio la ulipuaji bomu kulikuwa na tukio lingine la
ufyatuaji risasi.
Lakini bado hakujawa na ushahidi wa moja kwa moja kwamba nani alifyatua risasi na kwa sababu gani. Madai ya kufyatulia risasi watoto yana uzito wa pekee, pamoja na kutokuwepo kwa ushahidi wa moja kwa moja, vidole vingi vimekuwa vikinyooshwa kuwatuhumu polisi, kwamba risasi zilizofyatuliwa eneo la tukio zilitoka kwa polisi, na watoto walipigwa risasi na polisi.
Lakini bado hakujawa na ushahidi wa moja kwa moja kwamba nani alifyatua risasi na kwa sababu gani. Madai ya kufyatulia risasi watoto yana uzito wa pekee, pamoja na kutokuwepo kwa ushahidi wa moja kwa moja, vidole vingi vimekuwa vikinyooshwa kuwatuhumu polisi, kwamba risasi zilizofyatuliwa eneo la tukio zilitoka kwa polisi, na watoto walipigwa risasi na polisi.
Hata hivyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta
Jenerali Said Mwema tayari ameunda timu ya askari polisi kuchunguza
tukio hilo ambalo polisi wanatuhumiwa.
Kwanza tuweke wazi kwamba tuna imani kubwa na
utendaji kazi wa Jeshi Polisi, hivyo maoni yetu ni katika kujenga nyumba
moja kwa maana tukio la Soweto kwa watoto kupigwa risasi linahitaji
Tume Huru itakayokuwa na kada mbalimbali za wataalamu.
Tunaamini kuwa hata kama tume iliyoundwa na Mwema itafanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa, bado hali ya wasiwasi itaendelea kuwapo kwa kuwa polisi wananyooshewa kidole karibu na watu wengi.
Ni vyema Serikali ingeunda Tume Huru.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Tunaamini kuwa hata kama tume iliyoundwa na Mwema itafanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa, bado hali ya wasiwasi itaendelea kuwapo kwa kuwa polisi wananyooshewa kidole karibu na watu wengi.
Ni vyema Serikali ingeunda Tume Huru.
0 comments:
Post a Comment