Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM, Abdulhaman Kinana
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM, Abdulhaman Kinana amesema mfumo wa kijamaa umekua nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi nyingi duniani kwa kuwa ni mfumo unaopinga dhuruma na kuhimiza mshikamano katika kukua kwa maendeleo ya uchumi na hata sera.
Kinana ameyasema hayo katika mkutano wa chama hicho na kile cha kijamaa cha kutoka nchini Vietnam CPV uliofanyika jijini dare s Salaam, ukiwa na lengo la kuijengea uwezo CCM kutokana na uzoefu wa Vietnam ambayo imeongozwa na chama kimoja kwa muda mrefu sasa.
Akifafanua zaidi juu ya mkutano baina ya vyama hivyo viwili, Kinana ameongeza kuwa kwa miaka mingi kumekuwa na ukimya wa kimahusiano baina yao hivyo ujio wao unalenga kufufua uhusiano wa muda mrefu tangu mchakato wa kupatikana kwa uhuru wa nchi hii.
Mjumbe wa kamati kuu anayeshughulikia masuala ya kimataifa wa chama cha kijamaa cha Vietnamu CPV Bwana Hoang Binh Quan, amesema CCM imekuwa na mchango mkubwa katika ukombozi wa bara la Afrika kutokana na Sera nzuri za kijamaa zilizokuwa zikitekelezwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake.
Chama cha mapinduzi CCM, kimekua na mahusiano ya muda mrefu na chama cha CPV kutokana na mifumo na itikadi zake kiutawala kushabihiana na zikiwa na nia ya kupunguza matabaka ya kimaisha kati ya walionacho na wasionacho.
0 comments:
Post a Comment