Hali ilivyokuwa baada ya Msanii wa taarabu nchini Bi Khadija Kopa kupata taaarifa kuwa mume wake amefariki.
Khadija Kopa akilia kwa uchungu mara baada ya kupata taarifa za mumewe kufariki.
Akipewa sapoti wakati akielekea uwanja wa ndege.
Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar Kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jaffari Ally Yussuf aliyefariki dunia jana alfajiri. Bi Khadija Kopa alikuwa akitokea kwenye maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa juzi.
 
 Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, akilia kwa uchungu nyumbani kwake Tandale jijini Dar.

 Simanzi na majonzi vilitawala msibani hapo.
Akina mama waliofika kumpa pole Mama Mzazi wa Jaffari.

SIMANZI, vilio na majonzi vilitawala nyumbani kwa Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, Tandale jijini Dar. 

Marehemu Jaffari ambaye alikuwa ni mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa amefariki dunia usiku wa kuamkia jana  katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

 Marehemu Jaffari alikuwa Diwani wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati mama yake mzazi ni Mwenyekiti wa UWT Tandale.


 Mungu ailaze roho ya marehemu Jaffari Ally mahali pema peponi. AMEN!
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top