Waziri wa Afya, DK. Hussein Mwinyi.
Watanzania
wametakiwa kujenga utamaduni wa kupima afya za watoto na kupata elimu ya malezi
ya watoto hasa walio chini ya miaka mitano kwa ajili ya ukuaji wenye siha
njema.
Mkurugenzi
wa hospitali ya IMTU jijini Dar es Salaam Dakta Ali Mzige amewataka wananchi kujitokeza jumapili wiki
hii katika hospitali hiyo kwa ajili ya upimaji wa Afya za watoto walio chini ya
miaka mitano bila malipo yoyote.
Mkurugenzi
huyo amesema kuwa asilimia 42 ya watoto walio chini ya miaka mitano wamedumaa
kutokana na kukosa lishe mahususi kwa ajili ya ukuaji wa miili yao.
Takribani
watoto 130 walio chini ya miaka mitano hufariki dunia kila siku hapa nchini kutokana
na Utapiamlo yaani lishe duni hivyo kuhitajika jitihada za pamoja katika
kukabiliana na tatizo hilo.
Mkurugenzi
huyo amesema watoto wengi wana uzito pungufu,wengine wamekonda na kudumaa kimwili
na kiakili kutokana na lishe duni.
Utapiamlo
hapa nchini unaiweka Tanzania nafasi ya tatu barani Afrika kwa utapiamlo
kutokana na lishe duni,nchi inayoongoza ni Congo DRC ikifuatiwa na Ethiopia.
Cha
ajabu hapa nchini ni kwamba hata mikoa
inayozalisha chakula na matunda kwa
wingi pia imeathirika zaidi na ugonjwa wa Utapiamlo. Mikoa hiyo ni Morogoro, Mbeya,Tanga, Rukwa, Iringa na Manyara.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment