Wananchi wakitoroka kufuatia mapigano kati ya M23 na wanajeshi wa serikali.
Waasi wa M23, mashariki ya DRC, wamekubaliana
kusitisha mapigano ili kumruhusu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban
Ki-moon, kuzuru eneo hilo linalokumbwa na vita. Hii ni kwa mujibu wa
msemaji wa kundi hilo.
Bwana Ban amewasili mjini Goma , ambako, mtu mmoja aliuawa katika shambulizi la roketi, siku ya Jumanne.
Ban ameelezea wasiwasi kuhusu mapigano hayo mapya yaliyoanza hivi karibuni.
Awali rais wa benki ya dunia , aliahidi kutoa msaada wa dola bilioni moja kusaidia Congo na nchi majirani zake.
Mkuu wa benki ya dunia, Jim Yong Kim, ambaye pia
yuko ziarani DR Congo, alisema kuwa pesa hizo pia zitatumika kwa afya,
elimu, biashara na miradi ya kuzalisha umeme.
Takriban watu 20 wameuawa tangu Jumatatu katika makabiliano mapya kati ya serikali na waasi wa M23.
Haya yamekuwa makabiliano ya kwanza kati ya
pande zote mbili, tangu waasi wa M23 kuondoka Goma mwaka jana baada ya
kuuteka mji huo mwezi Novemba.
Ban anatarajiwa kukutana na wanachama wa kikosi
kipya cha umoja wa Mataifa ambacho kimeundwa ili kukabiliana na makundi
ya waasi katika eneo la Maziwa Makuu.
Ziara ya bwana Ban inakuja siku moja baada ya
benki ya dunia kuahidi msaada wa dola bilioni moja kusaidia kuimarisha
maendeleo katika eneo hilo, lakini pesa hizo zitategemea ikiwa pande
mbili zinazozozana zitatii mkataba wa amani utakapoafikiwa.
Eneo la Mashariki mwa DRC, limenaswa katika
miaka ishirini ya vita kati ya wanajeshi wa makundi ya waasi wanaaminiwa
kuungwa mkono na Rwanda pamoja na waliokuwa wahusika wa mauaji ya
Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.
Kuna matarajio mengi kuwa kikosi hicho cha UN kitaleta utulivu katika eneo hilo lenmye utajiri mkubwa wa madini.
Mapigano yanaendelea kati ya majeshi ya serikali
na waasi wa M23 katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.Mashambulio yamezidi katika makaazi ya raia.
Wapiganaji hao wa M23 walikuwa wameahidi kusitisha mapigano wakati wa ziara hiyo ya Ban Ki Moon.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment