Baraza la Mitihani la Tanzania linawatangazia watu wote wanaotaka kufanya mtihani wa kidato cha sita (ACSEE) mwezi Mei 2014 kama watahiniwa wa kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kitaanza rasmi tarehe 1 Julai, 2013 kwa ada ta shilingi 35,000/= na kipindi cha bila malipo kitaisha tarehe 31 Agosti, 2013.


Kuanzia tarehe 1 Septemba, 2013 hadi tarehe 30 Septemba, 2013 waombaji watajisajili kwa ada ya shilingi 50,000/= (Ada pamoja na faini).


Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti www.necta.go.tz ya Baraza la Mitihani la Tanzania.


Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji watapaswa kuchukua namba rejea (Reference number) katika vituo vya mitihani na watazitumia wakati wa kujisajili.


Hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila namba rejea kutoka katika kituo anakotarajia kufanyia mtihani.


Wakuu wote wa vituo nchini watakabidhiwa namba rejea kabla ya muda wa kujisajili kuanza na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo.

IMETOLEWA NA 
KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA 

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top