
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
24 MAY 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la Polisi Nchini
linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za
kiupelelezi kwa tuhuma za kueneza ujumbe wa uchochezi na chuki kwa
wananchi na viongozi wa serikali kwa njia ya simu ya mkononi akituma SMS
kwa lengo la kuchochea fujo, vurugu na kutoa matusi kwa viongozi hao.
Mtu huyo amekuwa
akifanikisha kazi hiyo kwa kutumia Chips (sim card) 13 za simu za
mkononi ambazo amekamatwa nazo. Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji mtu
huyo na ushahidi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
Jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuvunja sheria za nchi.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
0 comments:
Post a Comment