Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akionekana katika Sare zake za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).Picha hii inatajwa kupigwa Mwanzoni mwa Miaka ya 80 wakati huo Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Jeshini.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Anne Simamba Makinda katika Kivazi chake na Namna alivyotengeneza nywele zake.Picha hii ilipigwa Mwaka 1994 wakati Mama Anne Semamba Makinda akiwa ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania, Waziri wa Zamani wa Fedha, Mfanyabiashara na Mkulima Mashuhuri, Mchunga Mbuzi aliyebobea, Fundi Viatu aliyepata Elimu kwa Msaada wa Chama cha Ushirika, Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA na Mmoja wa Viongozi Madhubuti wa Taifa hili, Mzee Edwin Mtei.Picha hii ilipigwa Mwezi Aprili Mwaka 1974 wakati Bwana Edwin Mtei alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
 

Pichani ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda (wa Kwanza Kushoto) akiwa pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Bwana Christopher Ole Sendeka (Wa pili kushoto), Aliyekuwa Mkuu wa Mikoa Mbalimbali hapa Nchini, Bwana Ditopile Ukiwaona Mzuzuri (wa tatu kushoto) na wa mwanzo upande wa kulia ni Kijana wa Mjini William Vangimembe Lukuvi.Picha hii ilipigwa Miaka ya 80 wakati huo Vijana hawa wakiwa ni Viongozi wa Jumuia ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi. 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top