Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu
na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya
nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani.
Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na
za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya
usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo.
Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili,
2013.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, SUMATRA ilipokea maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabara yakiwemo makampuni ya usafirishaji abiria ya Cordial Transport Services P.L.C, Happy Nation Co. Ltd, ABC Trans na Mwesigwa Mtazaha Kazaula yakipendekeza mapitio ya viwango vya nauli za mabasi yanayotoa huduma za usafiri mijini (Daladala) na mabasi yanayotoa huduma katika Mikoa kufuatia ongezeko la gharama za uendeshaji kwa mujibu wa mawasilisho yao.
Wakati maombi ya wamiliki wa Daladala yalilenga katika kuongeza viwango vya nauli kwa 149% ya viwango vya sasa, wamiliki wa mabasi ya masafa marefu waliomba nyongeza kati ya 35% na 48.5%.
Kwa mujibu wa Kifungu Na 18 cha Sheria ya SUMATRA, 2001, SUMATRA iliwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu maombi ya wamiliki ya kuongeza viwango vya nauli kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.
Aidha Mamlaka iliridhia viwango vipya kwa mujibu wa kifungu cha 16 Cha Sheria ya SUMATRA ambacho kinaipa Mamlaka kufanya mapitio ya nauli mara kwa mara kwa kuzingatia gharama za kutoa huduma, maslahi ya watoa huduma, faida, maslahi ya watumia huduma ya kulipa nauli yenye uwiano na gharama za huduma inayotolewa.
Kwa kuzingatia hoja za waombaji, maoni ya wadau, uchambuzi wa menejimenti, haja ya kupunguza gharama zisizo za lazima za uendeshaji na udhibiti wa vitendo vya uvunjaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji shughuli za usafirishaji, Mamlaka ya SUMATRA iliamua kuongeza viwango vya juu vya nauli za Daladala kwa wastani wa 24.46%.
Aidha kwa mabasi ya masafa marefu, viwango vimeongezwa kwa 20.3% kwa mabasi ya kawaida, 16.9% kwa mabasi ya daraja la kati na 13.2% kwa mabasi ya daraja la juu.
1. Nauli za Daladala – Jiji la Dar es Salaam
Mamlaka imeandaa majedwali kwa njia zote za Dar es Salaam. Majedwali hayo yanaweza kupatika katika tovuti yetu www.sumatra.or.tz
Nauli ya Mwanafunzi itakuwa Sh 200/= ambayo ni nusu ya nauli ya mtu mzima ya kiwango cha chini cha nauli ya Sh 400/=. Nauli hii itatumika kwa njia zote za Jiji la Dar es Salaam.
2. Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu
Nauli ya Mwanafunzi itakuwa Sh 200/= ambayo ni nusu ya nauli ya mtu mzima ya kiwango cha chini cha nauli ya Sh 400/=. Nauli hii itatumika kwa njia zote za Jiji la Dar es Salaam.
2. Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu
li kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya
viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa
maagizo kwa wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuboresha maeneo
yanayohusiana na huduma ya usafiri kama ifuatavyo:
Aidha kwa mabasi ya mjini, Mamlaka imetoa maelekezo yafuatayo:
Mamlaka ya SUMATRA inaendelea
kuimarisha ushirikiano kwa kufanya kazi kwa karibu na Mamlaka zingine
kama Wakuu wa Mikoa, Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji, Polisi, TBS,
TANROADS, Kamisheni ya Bima na wananchi kwa ujumla, katika kuleta
mageuzi kamili ya utoaji wa huduma za usafiri wa barabara kwa kiwango
cha juu.
A.S.K. Kilima
KAIMU MKURUGENZI MKUU
2 Aprili, 2013
- Wamiliki wa mabasi kutokutumia wapiga debe katika kuuza tiketi za safari
- Wamiliki wa mabasi kuhakikisha wanafuata Kanuni za SUMATRA za Udhibiti wa Tozo na Nauli (SUMATRA Tarrif Regulations) ambazo zinahimiiza kuwepo kwa kumbukumbu sahihi za mahesabu ili kurahisisha mapitio ya viwango vya nauli
- Kufuata Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria
- Kutoza nauli kwa mujibu wa daraja la basi lenye sifa kamili la daraja husika kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Usalama na Ubora
- Kuhakiksha kuwa abiria wote wanapatiwa tiketi
- Kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria ikiwemo kutokamilisha safari maarufa kama kukata ruti, kubadili njia na unyanyasaji wa aina yoteyote kwa abiria
- Kutokutumia wapiga debe
- Wafanyakazi wa mabasi kuvaa sare nadhifu wakati wote.
A.S.K. Kilima
KAIMU MKURUGENZI MKUU
2 Aprili, 2013
2 comments:
TUMEUMIZWA KWA KWELI
Hivi haya ndio maisha bora tuliyoahidiwa au
Tunaomba kwa MAENEO ya Kivule,flemu kumi ,msongora Watu bado wanaumizwa Sana Kuna gari inafanya usafiri gerezani fremu kumi inatoza nauli mara mbili natiketi hatoi
Post a Comment