Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inawatangazia wamiliki wa Shule za Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu visivyo vya Serikali kuwa itafanya zoezi la kuhakiki uwepo wa Vyeti vya Usajili wa Shule na Vyuo vya Ualimu kwa Shule na Vyuo vilivyosajiliwa. 

Zoezi hili litaanza mwanzoni mwa mwezi wa Sita, mwaka 2013.

Wamiliki wa Shule na Vyuo vya Ualimu visivyo vya Serikali watapaswa kuonesha vyeti halisi vya Usajili wa Shule/Vyuo kwa watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi watakapofika kwenye Taasisi husika. Aidha, endapo shule yako imesajiliwa na hujachukua cheti cha Usajili, tafadhali wasiliana na Kitengo cha Usajili wa Shule, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Tafadhali toeni ushirikiano.

KAMISHNA WA ELIMU
13/03/2013
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top