Wanaume wanaoanza kuwa na upara huenda
wakakabiliwa zaidi na tisho la maradhi ya moyo kuliko wenzao waliojaa
nywele vichwani.
Hii ni kwa mujibu wa watafiti nchini Japan.
Utafiti huu uliowahusisha watu
37,000, ulichapisha taarifa kwenye jarida la mtandao, 'BMJ Open' ukisema
kuwa wanaume wanaokuwa na upara kwa asilimia 32 wanaweza kuwa na
maradhi ya moyo.
Hata hivyo, watatifi walisisitiza kuwa athari hizi ni chache ikilinganishwa na zile za uvutaji sigara na unene kupita kiasi.
Shirika linalojikita katika maswala ya maradhi
ya moyo nchini Uingereza, limesema kuwa wanaume wanapswa kujichunga
wasinenepe kupita kiasi kuliko kuchunga nywele zao.
Kuanza kukuwa na kipara ni kawaida ya maisha kwa
wanaume . Wengi kuanza kukuwa na upara wanapokuwa miaka 50 na asilimia
80 ya wanaume hao, hupoteza nywele wanapokuwa na umri wa miaka 70.
Watafiti katika chuo kikuu cha Tokyo, walidurusu
utafiti wa miaka mingi iliyopita, kuchunguza uhusiano uliopo kati ya
kuwa na upara na maradhi ya moyo.
Walionyesha kuwa nywele ambazo zilianza
kutoweka, zina uhusiano na maradhi ya moyo. Hii ilikuwa baada ya
kuzingatia maswala kama umri, na historia ya familia.
Daktari, Tomohide Yamada, wa chuo kikuu cha
Tokyo alisema kuwa walipata uhusiano mkubwa kati ya upara na tisho la
kupata maradhi ya moyo.
"tuliona hili kama jambo muhimu, lakini halina
athari kubwa kama mambo mengine yanayosababisha maradhi ya moyo kama
vile uvutaji sigara, unene kupita kiasi na mafuta mengi mwilini pamoja
na shinikizo la damu.''
Alisema kuwa wanaume wenye umri mdogo wanaopata
upara wanapaswa kuanza kuzingatia afya njema ili kujikinga kutokana na
maradhi ya moyo.
Aidha alisema hakuna ushahidi wa kutosha kupendekeza kuwa wanaume wenye upara wafanyiwe uchunguzi wa maradhi ya moyo.
Maradhi ya moyo ndio moja ya sababu kuu za vifo nchini Uingereza.
Mmoja kati yawanawake wanane kufariki kutokana na maradhi ya moyo.
Husababishwa na mishipa ya damu ambayo husukuma damu kwa moyo pale inapoziba.
Mmoja wa madaktari wakuu Uingereza amesema kuwa ingawa utafiti huu unaibua hisia, wanaume wenye upara hawapaswi kuwa na hofu.
Chanzo: BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment