Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatangaza orodha ya majina ya walimu wa shule za sekondari na vyuo vya ualimu waliopatiwa ajira awamu ya pili. Awamu ya pili ya ajira imejaza nafasi wazi zilizotokana na baadhi ya walimu kutoripoti katika vituo walivyopangwa katika ajira ya awali iliyotangazwa. 

Orodha ya majina ya walimu waliopangwa inapatikana katika tovuti zifuatazo: Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz ) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Utumishi.go.tz ). 


Walimu waliopangwa wanatakiwa kuripoti ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Vyuo vya Ualimu wakiwa na vyeti halisi vya taaluma na cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake ifikapo Aprili 30, 2013. Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo Mei 09, 2013 atapoteza nafasi hiyo na hatapata fursa ya kuajiriwa tena.

Aidha, Wizara inawakumbusha Walimu ambao walikuwa wameajiriwa na Serikali kabla ya kwenda masomoni kurudi katika vituo vyao vya kazi. Walimu watakaokiuka watachukuliwa hatua za kinidhamu na waajiri wao.

Tangazo hili limetolewa na:

Katibu mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
24/04/2013

Bofya kitufe husika hapo chini kupata majina unayotaka kupata.

icon AJIRA YA WALIMU WA SHAHADA AWAMU YA PILI (99.39 kB)

icon AJIRA YA WALIMU WA STASHAHADA AWAMU YA PILI (34.29 kB)
 
icon AJIRA YA WAKUFUNZI AWAMU YA PILI (16.76 kB)
Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top