Spika wa bunge Mh. Anne Makinda
Spika wa bunge Mh. Anne Makinda amelazimika kuahirisha
bunge hadi siku ya Jumatatu tarehe 29 ya mwezi wa nne na kuitaka serikali
kuiangalia upya bajeti hiyo baada ya wabunge wengi kukataa mapendekezo ya
bajeti hiyo iliyowasilishwa na waziri wa maji Profesa Jumanne Maghembe.
Wabunge wengi wametoa maoni yao wakidai bajeti ya
wizara hiyo ina mapungufu mengi yanayopelekea
kutokamilishwa kwa miradi mbalimbali ya
maji.
Miongoni mwa mambo yaliyokosolewa na wabunge ni ,ufinyu
wa bajeti na uchakavu wa miundo mbinu ya maji hivyo kuwakosesha wananchi huduma
hiyo muhimu ya maji .
Aidha wamesema wanaomba serikali kupeleka maji
vijijini kwa haraka ili kupunguza kero wanayoipata akina mama na watoto kwenda
kutafuta maji umbali mrefu na kuwafanya watumie muda mwingi kwenye kufuatilia maji.
Katika mawasilisho yake waziri mwenye
dhamana Prof. Jumanne Maghembe alisema tatizo la maji linachangiwa zaidi na
uharibifu wa vyanzo vya maji , ongezeko la idadi ya watu pamoja na uchakavu wa
miundombinu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment