Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa,  Profesa  Ibrahim Haruna  Lipumba

Kufuatia kauli zenye kuudhi kujitokeza mara kwa mara bungeni mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF taifa Profesa  Ibrahim Haruna  Lipumba amelitaka Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  kufuata kanuni na taratibu za kuendesha taasisi hiyo muhimu.

Profesa Lipumba amesema kutokana na mwenendo wa bunge wa kuzomea hovyo, kutovumiliana kutotii amri ya spika  na wabunge kutohudhuria bungeni lipumba amesema ni lazima bunge hilo liache ubabe na kutenda haki.

Aidha mwenyekiti huyo amesema ofisi ya spika ifuate sheria, kanuni na taratibu za bunge ili kujenga  misingi ya utawala wa haki na usawa katika kuliongoza bunge na kupunguza misuguano ya mara kwa mara inayojitokeza baina ya wabunge wa upinzani na chama tawala. 

Kiongozi huyo  amelitaka bunge kujikita katika kutetea maslahi ya wananchi badala  kutawaliwa na lugha ya kejeli na matusi kitu ambacho amesema hakiwezi kuwasaidia wananchi waliowachagua.

Katika  hatua nyingine profesa Lipumba ambaye pia ni mtaalam wa uchumi  ameitaka serikali kusikiliza madai ya wakulima wa korosho katika wilaya ya Liwale mkoani Lindi  ili kuepuka vurugu na machafuko yaliyotokea mapema Jumatano wiki hii.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top