Baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu na Mbunge wa Arusha mjini na uvamizi wa Polisi wakati wa usiku  wa manane, Mh. Lema alikubali kukamatwa na kuchukuliwa na gari la polisi usiku na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha yaani Central Polisi.


Kukamatwa  kwake  kulikuja  baada  ya polisi  kuvunja mlango na kuingia ndani  na  kuendesha  msako  wa  nguvu  humo  ndani .Vitu  kama laptop, ipad, simu vipo mikononi mwa police.
 
Wananchi wengi walijitokeza ku-support mbunge wao na huenda Asubuhi wananchi wakawa wengi zaidi.


Safari ya Lema  kuelekea  polisi  ilisindikizwa na msululu wa magari ya makada waliojitokeza kumsupport kuelekea kituo cha polisi.

Baada ya kumfikisha Lema Central police Arusha alisachiwa na kuingizwa ndani.  Lema alikuwa ameambatana na magari ya wafuasi wa Chadema waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni.

Baada ya  kumtupa  ndani, polisi waliwafukuza wafuasi  hao wa Chadema hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo.
Mpekuzi


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top